Sunday 23 May 2010

Kutoa ni moyo...............!



Nimerudi ndugu zangu, baada ya kufikiri kwa muda mrefu sana nipo tayari kushiriki nanyi. Nitatoa sababu za kuto kuwepo hewani kwa muda baadaye........, lakini sasa naomba tumuangalie kijana huyu na kila utakavyoguswa jaribu kusaidia.

jina: Noel G.shirima.
umri miaka 21
Elimu: ni mhitimu wa kidato cha nne, Katika shule ya secondari Mawela (Moshi - Kilimanjaro)Index number S1121/0115
M
NOEL G SHIRIMA
26
IV
CIV-C HIST-F GEO-D KISW-C ENGL-C PHY-F CHEM-D BIO-D B/MATH-F

Hakubahatika kuchaguliwa kujiunga na elimu ya secondari kwa kidato cha tano na sita katika shule za serikali, hali hii ilimhitaji kutafuta uwezekano wa kusoma katika shule nyingine (bianafsi). Nilipokutana naye kwa mara ya kwanza alikuwa mwanfunzi wakidato cha nne, nilistushwa na hali ya kwao kwani japo kuwa ipo duni sana kijana alikuwa mwenye furaha na nidhamu ya hali ya juu. Hapa ni nyumabani kwao, na hii ndo nyumba ya wazazi wake.


Nilifurahishwa na bidii na ubunifu wake, kwa muda mrefu amejilipia ada yake shuleni. Hili liliwezekana kwakuwa eneo analoishi lina tatizo la upatikanaji wa maji, na yeye aliamua kuanza kuuza maji, kwa shilingi 250 kwa ndoo, tatizo ni kwamba maji hayo yanapatikana mbali sana.

Aliamua kujijengea "kijijumba" chake ili kupisha nyumba ya wazazi wake, hapa akiwa nje ya kijinyumba hicho.


Kutokana na halo niliyoikuta kwao ilinibidi kuamini kuwa kijana anaakili na uwezo kwani pamoja na kuwa na hali duni kujitafutia mwenyewe ili kukidhi mahitaji yake na ya familia yake lakini ameweza kufanya vizuri baadhi ya masomo. katika mtazamo wangu sikudhni kama angepata hata credit (principal pass)moja.

Ninadhani anahitaji msaada, alipata kuitwa kujiunga na shule ya secondary Mombo, gharama zake zikawa kubwa mno kiasi ambacho ilibidi aje kuniona lakini sikuweza kumsaidia kwa kiasi kitakacho muwezesha kujiunga na shule hiyo.

Anahamu ya kusoma katika mazingira mazuri akiamini kuwa atafanya vizuri. Ndugu zangu nitaweka baadaye nakala ya barua ya kuitwa shuleni ikiwa na maelezo ya gharama zake, pia nita jitahidi kuwaona wazazi wake mungu akipenda nitaweka video za mazungumzo yao. natarajia pia kuweka namba ya simu, namba ya akaunti na ramani ya kufika kwao kwa atakayeguswa. Mungu awabariki.

Kutoa ni moyo...............

3 comments:

Mzee wa Changamoto said...

WOW!!!
Ni zaidi ya deni kusoma jitihada za mtu kama huyu na nia hasa ya kufanya afanyavyo.
Ni kama ilivyokuwa ile habari iliyoandikwa na Kaka Kamala na sasa hii yako kumhusu Kaka Noel.
Niliwahi ambiwa kuwa ukitembea vijijini unaweza kuwa mwendawazimu hasa baada ya kuona "matumbuzi" ya mjini.
Na huu ni moja ya mifano mingi halisi juu ya hili.

chib said...

Naaam, Mzee wa Changamoto, ni kweli kabisa. Kuna mtu kijijini, ukimpa 5,ooo anaweza kukuimbia hata wimbo wa Taifa, na akaweka jina lako pale linapotakiwa kutamkwa jina la nchi

Vimax Pills said...

Nice blog and article, thanks for sharing.