Tuesday, 3 November 2009

HII NI KAZI NZURI, kWA KIASI GAN?I

nI KAZI NZURI KUPITIA BLOGS, NI KAZI NZURI KUCHANGIA, KUTOA MAONI Je ni kwa kiasigani? wasiokuwa na uelewa wa komputer, uelewa wa matumizi , wasio na uelewa wa matumizi ya blogs wanapata manufaa ya kazi hii nzuri? Ndo kwanza naanza kutumia blog na nafurahishwa na kazi nzuriinayofanya lakini huu uzuri ni wa kiasi gani? Je ni wangapi wanaofaidi? je unaleta mabadiliko kwa kiasi gani?

7 comments:

Masangu Matondo Nzuzullima (MMN) said...

Kutokana na ugumu q upatikanaji wa kompyuta na mtandao, ni watu wachache wanaofaidika na blogs hizi. Lakini zipo chache ambazo zimeweza kufanikiwa sana mf. Michuzi, Mjengwa na zinginezo na zote ni kwa sababu mbalimbali lakini hasa ni kutokana na kufuatiliwa na Watanzania wengi waishio nje ya nchi.

Pia kama vile ilivyo katika magazeti na vitabu, watu wengi wanapenda habari za kusisimua, udaku, longolongo na blogu za aina hii pia zimefanikiwa/zilifanikiwa (unaikumbuka Ze Utamu?) Blogu nyingi zinazoandika makala za kiuchambuzi hazifanyi vizuri sana kwa sababu watu hawapendi kusoma habari ndefu na za kina. Hili tatizo lipo katika magazeti na hata vitabu. Mf. magazeti ya udaku yanafanya vizuri sana lakini yale yanayoandika habari za kina za kiuchambuzi hayasomwi sana.

Jambo hili hata hivyo halipaswi kutukatisha tamaa. Blogu hizi zinasomwa na ni wazi kwamba zinasaidia katika mijadala mbalimbali muhimu inayohusu mambo muhimu katika jamii yetu. Na kama tunavyosema katika masumbwi "one round at a time" basi hata kama tunaelimisha mtu mmoja "at a time" ni sawa. Karibu sana uwanjani na daima usikate tamaa kuhusu kusomwa au kutosomwa kwa blogu yako. Mapambano na uelimishaji wa jamii ni lazima uendelee!

Christian Bwaya said...

Anachokisema Profesa Matondo ni kweli. Kwamba tatizo tulilonalo nchini Bongo ni ukosefu wa utamaduni wa kujifunza (kwa kutumia viandikwa). Huenda si huduma yenyewe hasa ya internet inayokosekana.
Hivi sasa, kwa mfano kuna idadi kubwa ya watu ‘wenye habari’ na matumizi ya internet. Na kwa kasi hii, inawezekana kabisa tukawa mbali sana baada ya muda mfupi kwa maana ya kutapakaa huduma hii kwenye maeneo mengi zaidi nchini. Kuna simu siku hizi ambazo nazo zimeongeza wigo wa mtapakao wa huduma hii muhimu.
Hata hivyo kinachotia shaka ni matumizi yenyewe ya internet kwa hao watumiaji (wachache) hivi sasa. Wanaojitahidi, basi hutumiana barua pepe ambazo hawajaziandika wao. Yaani wanazipokea wao, na wao wanakumia wewe. Ukasuku fulani hivi, ambao nao ni hatua muhimu.
Wengine kazi kubwa ni kutafuta wapi wanaweza kupata mtandao wenye ladha ya ngono. Pamoja na ukweli kwamba bado gharama za kupata muda wa hewani nchini Bongo ziko juu, bado watumiaji wengi wanamudu kukaa masaa mengi sana mtandoni wakifanya vitu vya kipuuzi. Kwa hali hii, nadhani hata watanzania wote wangeanza kutumia internet leo, bado matumizi yasingeleta faida yoyote ya maana zaidi ya kubadilishana habari nyepesi nyepesi zisizombali sana na upuuzi.
Ukitaka kupata picha ya aina ya utamaduni tulionao watanzania kwa njia rahisi sana, chunguza blogu. Blogu zenye habari nyepesi ndizo zinazoalika idadi kubwa ya watembeleaji. Na kwa kweli kupata idadi kubwa ya watembeleaji si kazi ngumu sana. Hata wewe leo ukitaka blogu yako ijamu ndani ya wiki moja, ongelea masuala ya ngono na maisha ya watu maarufu. Weka picha za akina dada poa, anziasha topiki za kimapenzi; kwa mfano ‘ufanyeje ili upendeke...’. Simpo! Ni kihivyo tu, utashangaa idadi ya wasomaji itakavyokuwa kubwa pasipo mfano.
Lakini je, kipi muhimu? Kuandika ili kusomwa sana na wasiotaka kusoma, ama tuandike ili tusomwe na (wachache) wenye utaratibu wa kusoma? Je, tutajuaje idadi ya wasomaji wanaopitia blogu zetu? Ni kwa maoni yanayoachwa (maana kuna kautafiti nilifanya nikagundua mara nyingine maoni kadhaa huandikwa na mtu yuleyule) ama kusoma mita ya kurekodi wanaobofya kwenye blogu? Kwangu mimi nadhani tarakimu za ile mita si jambo la kujivunia/kukatisha tamaa (ndio maana sioni sababu ya kuwa nayo). Msomaji mmoja makini akikusoma anaweza kuongeza wasomaji wengi wasiotambuliwa na mita ya kwenye blogu.
Nadhani tuna kila sababu ya kuandika tunachooona kinafaa, bila kuzingatia wangapi watakisoma. Bora kuwa na wasomaji wawili (mmoja akiwa wewe unayeandika) ambao kwa hakika mnaweza kujadiliana vyema na mkajifunza mengi kuliko kuwa na wasomaji wengi ambao kazi yao kubwa ni kushabikia upuuzi.
Umefanya uamuzi sahihi kuanza kublogu. Itumie kuusemea moyo, hata kama tutakaosoma tutakuwa hawa hawa wa siku zote.

chib said...

Sasa mimi niseme nini tena, Bwanga na Matondo wamemaliza mpaka niliyotaka kusema mwakani.
Wasomaji wa blog wapo wengi, lakini sio wote hupenda kuchangia. Hata ukiona kimya, jua kuna watu wanapita kusoma mawazo yako.

chib said...

Sorry, nina maana ya Bwaya, na sio Bwanga!!!

Mzee wa Changamoto said...

Kwanza nikupongeze kwa kuanzisha BLOG. Pili niungane na watoa changamoto wenzangu kuhusu suala la kizazi chetu kisichopenda kufikirishwa. Ni KIZAZI TUNZCHOKIRITHISHA UJINGA wa UDAKU na habari za kizushi na TAARIFA zisizo na uchambuzi wowote.
Kuna faida kubwa kuwa na watu kama wewe na tupo Pamoja.
Blessings

Faith S Hilary said...

Faida zipo nyingi kaka ile point zote wamezisema kaka zangu hapo juu. Ila kila kitu kina uzuri na ubaya wake. So HONGERA kwa kuanzisha blog, sio kitu rahisi ila sio kama mtu hawezi kufanya. Just be yourself :-)!

Mch luv from candy1!xx

Obat Perangsang Wanita said...

Nice blog and article, thanks for sharing.